Kinara wa Chama cha ANC Musalia Mudavadi ametaka mikutano yote inayoendelezwa katika eneo la Magharibi mwa Kenya kusitishwa mara moja.
Kulingana na Mudavadi, mikutano hiyo inahatarisha maisha ya wakaazi wa eneo hilo kwani inawaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya Corona.
Mudavadi ameyataja makongamano hayo kama yanayoongozwa kisiasa na wala hayana agenda zozote za maendeleo kwa wakenya kama inavyodaiwa na maafisa wa Serikali.
Wakati uo huo amewakosoa Maafisa wa umma wanaoendelea kutumiwa kisiasa ili kuwahangaisha wakaazi wa Magharibi mwa Kenya na kuwataka wakaazi wa kanda hiyo kutoteteleshwa na hali hiyo.