Mtu mmoja anahofiwa kufariki baada ya jumba la ghorofa 8 kuanguka huko Malindi kaunti ya Kilifi.
Kulingana na baadhi ya wakazi walioshughudia kuanguka kwa jumba hilo, mkasa huo ulitokea alfajiri baada ya kusikika kwa mlipuko mkubwa. Nyumba hiyo inadaiwa imeanguka kutokana na mvua kubwa inayoshughudiwa katika eneo hilo.
Kwa mjibu wa mshirikishi wa shirika la msalaba mwekundu kanda ya Pwani, Hassan Musa amesema kuwa juhudi za ukozi zinaendelea huku tayari watu 8 wakiwa wameokolewa.
Taarifa na Charo Banda.