Picha kwa hisani –
Mtu mmoja amefariki papo hapo baada ya kuhusika kwenye ajali katika eneo la Likoni jioni ya leo.
Maafisa wa polisi katika eneo la Likoni wamesema ajali hiyo imehusisha pikipiki mbili zilizokuwa zimebeba abiria wawili wawili kila pikipiki na kisha kugongana ana kwa ana katika eneo hilo.
Hata hivyo abiria wote mmoja akapata majeraha mabaya kichwani na kufariki papo hapo huku wengine wanne wakikimbizwa hospitalini kwa matibabu ya dharura.
Polisi wamesema hakuna dereva wala abiria yeyote aliyekuwa amevalia kofia maalum ya kujikinga na majeraha yaani Helmet.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani.