Story by Charo Banda –
Hali ya taharuki na huzuni imetanda katika kijiji cha Takaye eneo la Malindi kaunti ya Kilifi baada ya mtoto mwenye umri wa miaka 7 kufariki dunia baada ya kugusa nyaya za umeme.
Juhudi za wakaazi wa kijiji hicho kumuokoa Mwanafunzi huyo wa darasa la kwanza kutoka shule ya kibinafsi ya Gloria Junior zimeambulia patupu baada ya kumpata tayari amefariki huku wakilaani vikali tukio hilo.
Kulingana na baba mzazi wa mtoto huyo Mwaro Mangi, mwanawe amefariki dunia alipokuwa akicheza nyuma ya duka moja kabla ya kugusa nyaza za umme zilizokuwa wazi.
Kwa upande wake Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Malindi John Kemboi amethibitisha tukio hilo, akisema tayari maafisa wa usalama wameidhinisha uchunguzi.