Takriban wanafunzi 408 kutoka shule 15 za msingi katika kaunti ya Kilifi wamelazimika kuufanyia mtihani wao wa kitaifa katika vituo vingine baada ya shule zao kuuathirika na mafuriko.
Akiongea na wanahabari baada ya kufungua rasmi makasha ya mtihani mapema leo kule Malindi mkurugenzi mkuu wa elimu kaunti ya Kilifi Eunice Khaemba amesema kuwa shule 10 zilizoathirika ni kutoka maeneo ya Ganze pamoja na shule 5 za eneo la Kauma.
Amesema kuwa wanafunzi hao wamehamishwa hadi eneo la Vitengeni ambapo ni kituo chenye nafasi za malazi na hata ni eneo ambalo haliwezi tatiza hali ya usafiri.
Mkurugenzi huyo aidha amesema kuwa kaunti ya Kilifi ina jumla ya wanafunzi 34,367 ambao wanaukalia mtihani wao wa KCPE huku kukiwa na jumla ya vituo 661 vya mtihani vilivyosajiliwa .
Vile vile Bi. Khaemba amefichua kwamba kaunti ya Kilifi ina jumla ya vituo 222 vya wanafunzi wa kidato cha nne ambao pia wanaendelea na mtihani wao wa KCSE.yaan practicals japo mtihani wenyewe utaanza wiki ijayo huku akiwaonya wanafunzi kujitenga na vishawishi vya udanganyifu