Biwi la Simanzi limegubika ulingo wa michezo nchini kufuatia kifo cha mtangazaji mkongwe wa soka, Mohammed Juma Njuguna.
Juma amefariki asubuhi ya leo katika hospitali ya Nairobi alipokuwa akipokea matibabu kwa muda.
Juma ni mmoja wa watangazi wakongwe wa mchezo wa soka humu nchini akibobea katika fani hiyo kwa miaka 40.
Mwaka wa 2010 alituzwa tuzo ya kitaifa na rais Mwai Kibaki.