Maafisa wa Polisi mjini Malindi kaunti ya Kilifi wanachunguza kisa kimoja ambapo raia mmoja wa Italia amepatikana akiwa amefariki ndani ya nyumba yake.
Kulingana na wakaazi wa eneo hilo, raia huyo wa kigeni anayefahamika kwa jina Alessandro Serezani mwenye umri wa miaka 80 alikuwa hajaonekana kwa jumla ya siku mbili kabla ya kupatikana amefariki kitandani mwake na akiwa anadamu kwenye mdomoni wake.
Kwa upende wake mlinzi wa makao hayo ya mtaliano huyo, Salim Omar amesema huenda alitumia sumu kujitoa uhai kwani awali alijaribu mara kadhaa kujitoa uhai kwa sumu lakini juhudi zake hakikufaulu.
Afisa mkuu wa uplelezi wa jinai eneo la Malindi Antony Sunguti amethibitisha kisa hicho, akisema tayari uchunguzi wa kina umeanzishwa huku mwili wa mwendazake ukihifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya kibinafsi ya Star mjini Malindi.
Taarifa na Charo Banda.