Waziri wa elimu nchini Balozi Amina Mohamed, ametangaza rasmi matokeo ya mitihani ya kitaifa ya darasa la 8 mwaka huu, mtahiniwa bora akijizoelea jumla ya alama 453.
Akitangaza matokeo hayo katika shule ya msingi ya Star of the sea jijini Mombasa, Balozi Amina amesema kwamba watahiniwa wawili wamepata alama hizo huku idadi ya watahiniwa waliopata alama 400 na zaidi ikiongezeka hadi 12, 273.
Amina aidha ametangaza kuwa watahiniwa wa kike wamewapiku wenzao wa kiume kwenye masomo ya Kiswahili, Kiingereza na lugha ya ishara, huku wakiume wakiongoza kwenye masomo ya hesabati, sayansi, somo la kijamii na somo la dini.
Habari zaidi kufuata hivi punde…