Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.
Mswada wa Punguza mzigo uliowasilishwa katika mabunge ya kaunti na chama cha Thirdway Alliance umezidi kutiwa dosari.
Akiyekuwa Katibu wa serikali ya Kaunti ya Mombasa Fancis Thoya amesema japo mchakato huo ni mwafaka, utabuni nafasi mpya za ajira kwa wanasiasa hali itakayochangia gharama kwa mlipa ushuru.
Kulingana na Thoya, mchakato huo unalenga kupunguza idadi ya viongozi, akihoji kwamba ni dhahiri Serikali kuu na zile za Kaunti zinamfyonza mlipa ushuru.
Akizungumza Mjini Mombasa, Thoya amehoji kuwa wakenya wengi wanaishi katika hali ya taabu kutokana na gharama ya juu ya maisha, akisisitiza ni sharti taifa hili liangazie zaidi kupunguza gharama ya maisha.