Story by Our Correspondent:
Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung’wa amepongeza mahakama kwa kuharamisha ushuru wa nyumba akisema uamuzi wa mahakama umetoa fursa ya kuidhinishwa sheria ya kuongeza ushuru unaokusanywa.
Akizungumza bungeni wakati akiwasilisha mswada wa nyumba za bei nafuu wa mwaka 2023 ili kujadiliwa kwa mara ya pili, Kimani amesema wameidhinisha vipengele vitakavyohakikisha wakenya katika sekta isiyo rasmi wanatozwa ushuru wa nyumba.
Hata hivyo wakati wa kujadili mswada huo wa nyumba za bei nafuu katika kikao cha bunge, majibizano yameshuhudiwa kati ya wabunge Kenya-kwanza na wale wa Azimio la umoja.
Mwakilishi wa kike kaunti ya Mombasa Zam zam Mohamed anayeegemea mrengo wa Azimio amesema serikali inawahadaa wakenya wenye kipato cha chini kwani hawawezi kumudu bei ya nyumba hizo zinazotajwa kuwa za bei nafuu.