Story by Rasi/Laurine-
Kijana wa umri wa miaka 28 amefikishwa katika Mahakama ya Kwale akikabiliwa na tuhuma za kunajisi mtoto wa umri wa miaka 16.
Mahakama imeelezwa kwamba mnamo tarehe 13 mwezi Februari mwaka huu, kijana huyo kwa jina Alex Mutunga alimnajisi mtoto huyo akiwa katika kijiji cha Kariryaka katika eneo la Kinango kaunti ya Kwale.
Mshukiwa akiwa mbele ya hakimu Joe Omido amekana shtaka hilo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 22 mwezi huu katika Mahakama hiyo.