Katika juhudi za kuwahimiza Vijana na jamii kuzingatia masharti ili kujikinga na virusi vya Corona, Vijana katika eneo la Mikindani Kaunti ya Mombasa wakumbatia mbinu ya muziki katika kuielimisha jamii kuhusu virusi hivyo.
Vijana hao wakiongozwa na Mwakilishi wa Wadi hiyo Juma Renson Thoya wamesema muziki umebainika kuwa mbinu inayowavutia vijana kupata ujumbe kwa njia wanayoielewa.
Kwa upande wake, thoya aliyeongoza hafla ya uzinduzi wa kibao cha Corona kutoka kwa msanii Justus Naftali kwa Jina maarufu Sharp Delamare amewasihi vijana kujitosa katika kampeni ya kuihamasisha jamii kuhusu athari za virusi vya Corona kwa kutumia sanaa na vipaji vyao.
Kwa upande wake, Msanii ‘Sharp Delamare’ amewahimiza Vijana na jamii kwa jumla kuzingatia masharti yote ya kiafya ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona.