Picha kwa hisani
Mwanamuziki kutoka Nigeria Peter Okoye maarufi Kama Mr.P na aliyekuwa katika kikundi Cha P Square na pacha wake, ameeleza kuwa yeye na mkewe pamoja na binti wao walipatikana na virusi vya Corona wiki 3 zilizopita.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, mwanamuziki huyo amechapisha video kadhaa akimshukuru Mungu kuwa yuko hai pamoja na familia yake baaada ya kupitia wakati mgumu Sana. Mr P pia alifichua kuwa wafanyakazi wake wawili wa nyumbani waliathirika na ugonjwa huo wa Covid 19 mapema mwezi huo.
“Kwa kipindi Cha wiki tatu, nimepitia hali ngumu na wengi hamkujua mbona nilikuwa nimekimya, niliona niiweke siri, nimekuwa na virusi vya Corona, mke wangu pia alipatikana na virusi hivyo,” – Mr P
Mr.P alieleza kujutia kumletea mwanawe virusi hivyo hatari vya corona na kwa sasa anaendelea na matibabu.
“Nilipatikana na maambukizi ya Covid 19 na nikawekwa karantini, singeweza kumuona binti yangu mgonjwa, hii ilinifanya nijisikie vibaya sana, najutia sana kumletea ugonjwa huu hatari,” -Mr.P
Hata hivyo, mkewe Lola hakupatikana na virusi vya corona baada ya kufanyiwa vipimo baada ya kuondoka karantini.