Story by Correspondents –
Msanii maarufu wa nyimbo za asili ya mijikenda Bin Kalama ameaga dunia.
Familia ya mwendazake imethibitisha kutokea kwa kifo cha msanii huyo siku ya Jumatano alasiri baada ya kuugua kwa mda.
Hata hivyo baadhi ya Wasanii wa nyimbo mbalimbali, wamesema kifo cha Bin Kalama ni pigo kwa sekta ya Sanaa ya mziki kwani nyimbo alizoimba zilibadili tabia za vijana wengi na kuwawezesha kuwa na maadili.
Bin Kalama atakumbukwa na wengi kwa nyimbo zake alizoimba kama ile ya I love you my darling, Ukongo wa nyerenyere miongoni mwa nyimbo zengine za asili ya mijikenda.