Picha Kwa Hisani
Wanamuziki tajika pamoja na mashabiki wa mwanamuziki maarufu kutoka nchini Uganda Juliana Kanyamozi wamemiminika kwenye mitandao ya kijamii kumpa hongera mwanamuziki huyo ambaye amejifungua mtoto wa kiume siku ya jumatano.
Msanii huyo maarufu kwa wimbo wake aliouimba na mwanamuziki Kidum kutoka nchini Tanzania ‘Mapenzi’alieleza furaha yake na habari hizo njema kwa ulimwengu kupitia mtandao wa Twitter. Kupitia post yake, Juliana pia alisema jina la mtoto wake huyo ambalo ni ‘Taj’.
Wanamuziki maarufu nchini humo Jose Chameleon, Weasel na Benda waliwaongoza wasanii wengine kumpa hongera Juliana kupitia mtandao huo wa Twitter. Mashabiki wake nao walimpongeza kwa kuuweka uja u zito wake kama siri hadi motto kuzaliwa.
Taj ni mtoto wa pili wa msanii huyo mwenye umri wa miaka 39. Mtoto wake wa kwanza, Keron Raphael Kabugo, alifariki dunia Julai 2014 akiwa na umri wa miaka 11 kufuatia ugonjwa wa pumu.