Msanii wa Bongo Fleva aliyevuma kwa kibao “nakupenda tu” Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya amekubali kuubeba msalaba.
Dudu Baya kwa muda mrefu amefahamika kama msanii mwenye vurugu na aliyekuwa na chuki na mastaa wengi wa mziki.
Akizungumza na wanahabari punde tu baada ya kupeana maisha yake kwa Yesu Kristo Dudu Baya amesema kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kugundua kuwa yuko na maadui wengi.
“Unajua maisha ni safari ndefu nimekuja kungundua kuwa nipo na maadui wengi sana. Kwa hiyo nikahitaji ulinzi zaidi na mimi siwezi kwenda kwa waganga ndio maana nikaamua kupata kinga ya ukweli ambayo ni damu ya Yesu Kristo,” amesema msanii huyo.
Aidha amesema kuwa kwa sasa maisha yake yamebadilika na atazidi kuwa na maisha mapya.