Tume huru ya uchaguzi na mpaka nchini IEBC imemtangaza mgombea huru wa uchaguzi mdogo wa ubunge wa Msambweni Feisal Abdallah Bader kuwa mbunge wa Msambweni baada ya kujizolea jumla ya kura 15, 251.
Afisa wa Tume ya IEBC anayesimamia uchaguzi huo Yusuf Abubakar Mohammed amesema Feisal ameibuka mshindi wa uchaguzi huo akifuatwa karibu mno na mpinzani wake Omar Idd Boga wa chama cha ODM aliyepata kura 10,444.
Akimkabidhi cheti chake Feisal, Yusuf amesema japo uchaguzi huo umeshuhudia purukushani ,usalama uliimarishwa na zoezi la upigaji kura likaedelea kwa amani.
Hata hivyo Shee Mahmoud Abdulrahman wa chama cha WIPER ameshikilia nafasi ya tatu baada ya kupata kura 790 huku nafasi ya nne akiwa Marere Wa Mwachai wa chama ha NVP kwa kura 300.
Hamisi Mwakaonje Liganje chama cha United Green Movement amepata 230, Charles Bambi Bilal ambaye nj mgombea huru akipata kura 135, Ali Hassan Mwakulonda wa chama cha PED kura 107, Sharlet Akinyi Onyango ilie mgombea huru kura 18 na Mansury Kumaka Abdulrahman kura 38.
Hata hivyo uchaguzi huo umejumulisha jumla ya kura 27,313 zilizopigwa ambayo ni asilimia 39.58 za kura zilizopigwa, 139 zilikataliwa, licha ya sajili ya wapiga kura kuwa 69,003.