Picha kwa hisani –
Wajumbe wa nchi wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wanakutana mjini New York baadaye leo kumchagua mwendesha mashitaka mpya wa mahakama hiyo.
Wagombea tisa ikiwa ni pamoja na majaji wawili mmoja kutoka Nigeria na mmoja kutoka Uganda, wako katika orodha ya kumrithi Bi Fatou Bensouda wa Gambia, ambaye muhula wake kama Mwendesha mashitaka wkuu wa mahakama ya ICC unamalizika mwezi Juni mwaka huu.
Bi Bensouda amekuwa Mwendesha mashitaka Mkuu wa ICC tangu mwaka 2011- baada ya kuchukua nafasi ya wakili Muargentina, Luis Moreno Ocampo.
Katika muhula wake madarakani, aliweza kuwatia hatiani washitakiwa Zaidi kuliko mtangulizi wake-wa hivi karibuni akiwa ni muasi wa zamani wa Uganda kamanda Dominic Ongwen ambaye mwezi huu alipatikana na hatia za uhalifu wa kivita.