Story by Hussein Mdune –
Mgombea wa kiti cha uwakilishi wadi ya Puma katika kaunti ya Kwale Mrinzi Nyundo ameihimiza idara ya usalama nchini kuweka mikakati mwafaka ya kuhakikisha usalama unaimarishwa wakati huu siasa za uchaguzi mkuu.
Mrinzi ameweka wazi kwamba kwa sasa visa vya utovu wa usalama vinashuhudiwa katika sehemu mbalimbali za nchi hivyo basi kuna haja ya usalama kuimarishwa ili kufanikisha uchaguzi wa amani.
Hata hivyo amewahimiza wakaazi wa Puma na kaunti ya Kwale kwa ujumla kujitenga na siasa za ukabila na badala yake kuungana kama wakenya sawa na kudumisha amani.
Wakati uo huo amewataka wakaazi wa wadi ya Puma na Kwale kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika zoezi la usajili wa wapiga kura.