Mradi wa kuwakimu vijana kwa ufadhili wa kibiashara unaonuiwa kuidhinishwa na benki ya dunia humu nchini kwa kiwango kikubwa utaibadili hali ya maisha ya vijana katika Ukanda wa Pwani amesema msimamizi wa msimamizi mkuu wa kituo cha teknolojia na sanaa cha ‘Swahilipot-Hub’ Mahmoud Noor.
Kulingana na msimamizo huyo anayesimamia mradi wa ‘Mbelenabiz’ ni kwamba mbali na ufadhili wa mtaji wa hadi shilingi milioni 3.6 kwa mradi wa kibiashara, vijana pia watafunzwa jinsi ya kuandika mpangilio maalum wa kibiashara ili kupata ufadhili zaidi.
Kulingana na Mahmoud, kituo hicho cha Swahilipot-Hub kimewekeza zaidi katika kuwahamasisha na kuwasaidia vijana kuandika mipangilio bora zaidi ya kibiashara ili biashara zao zipate ufadhili huo ambao hautamhitaji kijana kuzilipa fedha hizo.
Akizungumza katika kituo hicho cha ‘Swahilipot-Hub’ Mjini Mombasa hii leo, Mahmoud amewarai Vijana kuing’ang’ani nafasi hiyo ili wapate ufadhili wa kuidhinisha miradi yao ya kibiashara.