Picha kwa hisani –
Katibu mkuu msimamizi wa Wizara ya Vijana na michezo nchini Bi Nadia Abdallah, amesema mradi wa kuwaajiri vijana kupitia mfumo wa kidijitali maarufu Ajira Digital umewakimu vijana wengi kwa ajira nchini.
Akizungumza mjini Mombasa Nadia amesema ni sharti vijana wa Pwani kuikumbatie hali hiyo na wala sio kujitenga na nafasi hizo ambazo zinawanufaisha vijana wengine.
Amesema Serikali inawalenga Vijana milioni moja angalau kila mwaka kupitia mradi huo akiwataka vijana wa Pwani kushiriki kikamilifu mpango huo.