Mradi wa kuwapatia sindano safi waraibu wa dawa za kulevya wakujidunga kwa kiwango kikubwa umepunguza maambukizi ya virusi miongoni mwa waraibu hao.
Akizungumza Mjini Mombasa afisa anayeangazia afya ya watumizi wa dawa za kulevya kutoka Shirika la kupambana na utumizi wa dawa za kulevya la Reachout Centre Trust Pili Saria, amesema kwamba waraibu wanaojidunga wamo katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi kutokana na kutumia sindano moja kwa waraibu wengi.
Saria amesema kuwa mradi huo unaofahamika kama ‘Needle and Syringe Exchange Program’ umechangia pakubwa kupunguza maambukizi ya virusi na pia umewaleta waraibu karibu na washauri ili wasaidiwe kujinasua.
Mwanaharakati huyo amesema kuwa iwapo serikali kuu na zile za kaunti zitaupa mradi huo uzito unaostahili utasaidia kupunguza maambukizi ya virusi miongoni mwa waraibu katika Ukanda wa Pwani.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni