Picha Kwa Hisani –
Wanaharakati wa masuala ya kijamii katika kaunti ya Kwale wamesema hamasa zilizotolewa kwa jamii kupitia mpango wa hedhi salama zimesaidia kupunguza mimba za utotoni ndani ya Kaunti hio.
Wakiongozwa na Bi Christine Mvurya wanaharakati hao wamesema kupitia hamasa hizo jamii imevunja kimya na kuzungumza wazi wazi kuhusu suala hilo hali ambayo imepelekea visa vya mimba za utotoni kushuka.
Bi Christine amesema mwaka huu wameandikisha chini ya visa elfu mbili vya mimba za utotoni ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo zaidi ya watoto wa kike elfu tano walipata uja uzito.