Moto mkubwa umeteketeza trekta moja la kunyanyua makasha yaani ‘Folk lift’ katika bandari ya Mombasa jioni ya leo.
Haijabainika wazi kiini cha moto huo kilikuwa kipi japo shughuli za kuuzima moto huo zimeanza mara moja ili kuudhibiti moto huo kabla ya kusambaa katika makasha.
Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na usimamizi wa bandari hiyo kuhusu chanzo cha moto huo wala thamani ya mali iliyoharibiwa.
Hata hivyo, moto huo mkubwa umezimwa baadaye baada ya wazima moto katika bandari hiyo ya Mombasa kufika mara moja katika eneo hilo la mkasa.