Hali ya taharuki imezuka huko Malindi eneo la Casuarina baada ya moto mkali kuteketeza majumba mawili ya kibinafsi maarufu mapema leo.
Kulingana na Mchika Ndurya ambaye ni mmoja wa wakaazi walioshughudia Mkasa huo , moto ulizuka katika nyumba moja kabla ya kusambaa hadi nyumba ya pili.
Wakaazi hao wanadai kuwa huenda moto huo ulizuka kutokana na hitilafu ya nguvu za umeme.
Hata hivyo moto huo ulidhibitiwa kwa usaidizi wa majirani sambamba na maafisa wa zima moto waliofika eneo la Mkasa kwa wakati onaofaa.
Taarifa na Charo Banda.