Mali ya thamani ya mamilioni ya pesa imeharibiwa jioni ya leo baada ya moto mkubwa kuliteketeza bohari moja ya kuhifadhi bidhaa mbalimbali katika eneo la shimnazi Mjini Mombasa.
Moto huo umeliteketeza bohari hilo la rangi na biadha nyinginezo za ujenzi ka ‘Mamujee Hardware and Gerneral Stores’ mkasa uliyoanzia mwendo wa saa kumi jioni ya leo.
Imewalazimu wazima moto kutoka Serikali ya Kaunti ya Mombasa, Bandari ya Mombasa, jeshi la wanamaji la Navy na Shirika la kibinafsi la Jaffery Foundation kukita kambi ili kukabiliana na moto huo mkubwa.
Hapo awali mkasa huo umesemekana kuathiri eneo la makasha la AutoPort linalomilikiwa na gavana wa Kaunti ya Mombaa Ali Hassan Joho japo polisi wakathibitisha kwamba ni bohari hilo la Mamujee pekee lililoteketea.
Kamanda mkuu wa polisi wa Kaunti ya Mombasa Johnston Ipata ameongoza oparesheni hiyo akishirikiana na wanajeshi na Maafisa wautawala ili kuzuia mikasa zaidi au wizi wa mali kufuatia harakati hizo.
Hadi mwendo wa saa mbili na nusu usiku, moto huo ulikuwa bado haujadhibitiwa.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.