Maafisa wanaoshughulikia masuala ya watoto katika eneo la Kinango kaunti ya Kwale wamesema asilimia kubwa ya watoto eneo hilo wameshurutishwa na wazazi wao kutafuta ajira
Wakiongozwa na Monica Ndaro ambae ni afisa wa kujitolea amesema hali hio imechagiwa na hatua ya wazazi kukosa ajira kipindi hiki cha Corona na kukosa namna ya kukimu familia zao.
Bi Ndaro vile vile amesema visa vya watoto kudhulumiwa kingono na wazazi wao eneo hilo vimekithiri kutokana na hatua ya wazazi kujiingiza katika utumizi wa dawa za kulevya.
Afisa huyo wa kushughulikia masuala ya watoto eneo la Kinango hata hivyo ameitaka jamii kuhakikisha watoto wako katika mazingira salama badala ya kuwanyanyasa.