Picha kwa hisani –
Msimamizi wa serikali ya kaunti ya Mombasa katika eneo bunge la Changamwe Hezron Katana amewataka wakaazi wa kaunti hio kujizatiti na kudumisha usafi wa mazingira katika maeneo yao.
Akihutubia wakaazi wa eneo bunge hilo Katana amesema wakaazi wa kaunti ya Mombasa hawapaswi kuachia serikali ya kaunti hio jukumu la kusafisha miji ya kaunti hio.
Katana amesema serikali ya kaunti ya Mombasa tayari imeidhinisha mpango wa kusafisha mji wa Mombasa kila mwezi zoezi litakalojumuisha wadau mbali mbali ikiwemo wa mazingira.