Mahakama huko Malindi imemuachilia kwa masharti aliyekuwa msimamizi wa ghorofa iliyoporomoka mjini Malindi ambaye pia ni mwanawe mmiliki wa jengo hilo aliyefariki wakati wa mkasa.
Shabbir Ali Fakhruddin ameachiliwa kwa bondi ya shilingi laki tano, huku Mahakama ikipinga ombi la idara ya upelelezi kutaka mshukiwa huyo kuzuiliwa kwa siku 21.
Baadhi ya masharti yalitotolewa na Mahakama kwa mshukiwa ni pamoja na mshukiwa kutokaribia eneo la mkasa, kutotatiza ushahidi, kuripoti katika idara ya Upelelezi (DCI) kila anapohitajika, kuhakikisha anaishi mjini Malindi ili kupatikana kwa urahisi na kuhakikisha anaripoti kwa OCS iwapo anataka kutoka nje ya mji wa Malindi.
Hata hivyo mshukiwa huenda akakabiliwa na mashtaka ya mauaji sawia na kusababisha majeraha endapo atashtakiwa baada ya uchunguzi kukamilika. Idaya ya upelelezi imepewa hadi tarehe 19 mwezi wa Novemba mwaka huu kukamilisha uchunguzi ambapo kesi hiyo pia itatajwa.
Taarifa na Charo Banda.