Picha Kwa Hisani.
Mwanamuziki Mlole Classic anaendelea kupata afueni baada ya kupata ajali ya barabarani jijini Nairobi wikendi iliyopita.
Mlole alipata ajali baada ya pikipiki aliyokuwa anasafiria kugongana na matatu alipokuwa ametoka kwenye mahojiano kwa kituo kimoja cha radio Nairobi akielekea SGR kwa ajili ya kusafiri kurudi mjini Mombasa.
Mkali huyo wa ngoma ya “Zuzu” na anaye fanya vizuri ndani na nje ya Pwani, ameeleza kuwa anaendelea kupata afueni kwani hakupata majeraha mabaya.
Tunamtakia Mlole Classic afueni ya haraka.