Picha kwa hisani –
Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC imezindua mpango wa kuwahamisha wananchi wake katika mji wa mashariki wa Goma baada ya mlipuko mkubwa wa volkano kushuhudiwa katika mlima Nyiragongo.
Taarifa kutoka serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imesema chemichemi za lava zililipuka kutoka mlima huo na kuingia angani usiku wa kuamkia leo na kutengezena wingi zito la moto juu ya mji wa Goma ambao una idadi ya watu milioni mbili.
Mlimo huo wa Nyiragongo ulio na volkona uko maili sita kutoka kwa mji wa Goma na ulilipuka mara ya mwisho mwaka wa 2002 ambao wakati huo ulisababisha idadi ya watu 250 kuaga dunia huku watu laki moja na elfu ishirini wakikosa makaazi.
Japo haijabainika iwapo kuna idadi ya watu wameangamia baada ya mlipuko huo mkubwa wa Volkano, tayari mamia ya watu wameonekana kuhama mji huo na kuelelekea taifa jirani la Rwanda.
Hata hivyo serikali ya Rwanda imesema tayari raia elfu tatu wa taifa la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wameingia nchini Rwanda kutafuta hifadhi.