Mkurungezi wa Kituo cha habari cha Radio Kaya Rose Mwakwere amewapongeza wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya Kwale kwa kuibuka mabingwa katika mashindano ya soka ya shule za upili kanda wa Afrika ya Mashiriki.
Akizungumza na Wanafunzi hao walipokitembelea kituo cha Radio Kaya, Rose amesema ufanisi wa wanafunzi hao umeiweka kaunti ya Kwale katika hadhi ya kitaifa na kimataifa na wanafunzi hao wanafaa kupongezwa.
Aidha amewahimiza wanafunzi hao kuzingatia nidhamu shuleni ili kuwa kielelezo chema kwa wanafunzi wenzao na hata katika jamii.
Kwa upande wake mkufunzi wa timu ya wanafunzi hao, Mukasa Amboko ameeleza jinsi walivyojituma katika kuibuka washinda kwenye mashindano hayo ya kimataifa.
Naye Afisa wa miradi katika Shirika la Plan International, Harriet Osimbo amehimiza umuhimu wa jamii kuwalea watoto wao katika mazingira bora ili kuwaepusha na visa vya mimba za mapema.
Taarifa na Radio Kaya.