Picha kwa hisani
Mashabiki wa mwigizaji maarufu wa filamu za Nollywood, Regina Daniels, wameonyesha furaha kupitia mtandao wa Instagram baada ya mke mwenza wa muigizaji huyo kwa jina Laila Nwoko kumpa kongole baada ya kujifungua mtoto wa kiume.
Regina mwenye umri wa miaka 20 aliolewa na mwanasiasa maarufu Ned Nkowo mwenye umri wa miaka 60 mwaka wa 2019 kwenye harusi ya kufana na amejaliwa mtoto wake wa kwanza wa kiume siku chache zilizopita.
Laila ambaye ni raia wa Morocco, alimuandikia ujumbe huo wa kongole kupitia ukurasa wake wa Instagram masaa chache baada ya mume wao Prince kupost picha yake akiwa amamtembelea Regina hospitalini.
“Hongera Regina Daniels kwa kujaliwa mtoto wako wa kwanza,” – Laila aliandika Instagram.
Bila kusita, Regina alimshukuru Laila kwa kumtakia heri njema na pia kuelezea kuwa anampenda sana.
“Asante sana Laila…., nakupenda sana,” Regina alimjibu.
Wawili hao wamethibitisha kwa umma kuwa licha ya kuwa katika ndoa ya mitala, wanapendana na wamekubali kuishi aina hiyo ya maisha. Regina kwa mara kadhaa ameonekana akiwa na wakati mzuri na watoto wa Laila ambao bila shaka pia wanampenda mwigizaji huyo.