Kipindi cha Kaya Flavaz kimepata sauti mpya.
Ni sauti ya kike itakayokunoga kila siku ya juma kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana.
Ni sauti ya mrembo Caroline Mkamburi.
Mrembo huyo atakuwa anaendesha kipindi hicho bora hapa mwambaoni na Robby Dallaz.
Kando na Mkamburi vilevile kipindi hicho kimepigwa jeki katika upande wa utafiti. Mwajenjewa Suleiman atahusika katika kitengo cha utafiti katika kipindi hicho.
Vilevile watatu hao watahusika katika kipindi cha Kali Zetu ambacho hivi sasa kitaanza saa nne asubuhi kila siku ya jumamosi hadi saa tisa mchana.