Picha kwa hisani –
Mitihani ya majaribio kwa wanafunzi wa gredi ya nne na darasa la nane iliopangwa kufanyika hii leo katika shule za msingi kote nchini imesongezwa mbele hadi siku ya jumatano juma hili.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari,afisa mkuu mtendaji wa baraza la mitihani nchini KNEC Mercy Karogo amesema kuhairishwa kwa mitihani hio kunalenga kutoa nafasi kwa sherehe za mashujaa zitakazofanyika hapo kesho.
Kerogo amesema mitihani hio sasa itafanyika kati ya tarehe 21 hadi tarehe 26 mwezi huu wa Oktoba,akiwata waalimu katika shule za humu nchini kufanya matayarisho ya kutosha kwa ajili ya mitihani hio.
Ameshikilia uamuzi wake wa hapo awali kwamba ratiba ya mitihani kwa wanafunzi ambao wako nyumbani kwa sasa itatolewa punde wanafunzi hao watakaporejea shuleni.