Mbunge wa Likoni Bi.Mishi Mboko amesema kuwa ajenda nne kuu za serikali kuu zitafanikishwa iwapo wananchini watakoma kubaguana katika misingi ya kidini na kikabila.
Bi.Mboko amesema mivutano ya kisiasa na kikabila inayoshuhudiwa miongoni mwa Wakenya imeathiri pakubwa ustawi wa taifa.
Mbunge huyo wa Likoni amewataka wakenya sawia na viongozi, kukoma kulumbana kila mara na badala yake kushirikiana katika kufanikisha maendeleo ya kitaifa.
Bi.Mboko amefichua kuwa atafanya kazi kwa ukaribu na viongozi wakuu serikalini, ili kuhakikisha wakaazi wa Likoni na kaunti ya Mombasa kwa jumla, wananufaika na maendeleo.
Taarifa na Hussein Mdune.