Mbunge wa Likoni Bi Mishi Mboko amehimiza ushirikiano wa wazazi na viongozi katika eneo hilo kukuza talanta na vipaji vya vijana ili kuwawezesha kujibunia ajira.
Akizungumza huko Likoni, bi Mboko amesema kuwa chanzo cha vijana wengi kujihusisha na uhalifu katika kaunti ya Mombasa na kote nchini ni ukosefu wa ajira.
Bi. Mboko ametaja kwamba ushirikiano wa wazazi na viongozi kukuza talanta za vijana, utasaidia pakubwa kukabili ukosefu wa ajira.
Mbunge huyo wa Likoni ametoa changamoto kwa viongozi nchini kulipa kipaumbele suala la ajira kwa vijana akisema kwamba zaidi ya asilimia 70 ya vijana nchini wanaishi maisha magumu kwa kukosa ajira.
Kauli ya kiongozi huyu imejiri huku visa vya vijana wenye umri mdogo kujihusisha na uhalifu vikiongezeka katika eneo la Likoni na Kisauni.
Taarifa na Hussein Mdune.