Picha kwa hisani –
Mbunge wa Likoni Bi Mishi Mboko amesema suala la usawa wa jinsia linastahili kushughulikiwa kupitia kufanyiwa marekebisho kwa katiba ya nchi.
Akizungumza na mwanahabari wetu Bi Mboko amesema katiba ya mwaka 2010 imejumuisha kipengele kinachoangazia usawa wa jinsia,na ni kupitia marekebisho ya katiba ndipo wakenya wataamua iwapo kipengele hicho kifanyiwe mabadiliko au la.
Bi Mboko amesema anaunga mkono marekebisho ya katiba kupitia BBI akisema ni kupitia mchakato huo ndipo vipengele vyenye utata katika katiba ya nchi vitabadilishwa na kumaliza mvutano wa kikatiba nchini.
Kauli yake inajiri huku kukiwa na shinikizo za kuvunjwa kwa bunge kwa kushindwa kupitisha sheria ya tuuthi mbili ya usawa wa jinsia.