Mbunge wa Kandara Alice Wahome amezidi kukosolewa kufuatia madai yake kwamba mpango wa BBI unalenga kuwaeka baadhi ya wanasiasa uongozini akiwemo Rais Uhuru Kenyatta baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2022.
Wa hivi punde kumkashfu Bi Wahome ni Mbunge wa Likoni Bi Mishi Mboko aliyemtaka Bi Wahome kutozua mijadala inayolenga kuligawanya taifa badala ya kuunga mkono mchakato wa kuunganisha.
Mboko hata hivyo amesema uamuzi wa muongozo tofauti wa taifa hili umo mikononi mwa wakenya na wala sio wanasiasa wachache.
Kauli ya Mboko inajiri baada ya Mbunge huyo wa Kandara Kaunti ya Murang’a Bi Ali Wahome akiwa kule Mjini Malindi juma lililopita kuweka bayana kwamba jopo kazi la maridhiano BBI linalenga kuwaeka Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM Raila Odinga uongozini na haina malengo ya kuwaunganisha Wakenya.