Story by: Gabriel Mwaganjoni:
Japo kumekuwa na changamoto hasa ya kupata maji ya kuikuza miti katika juhudi za upanzi wa miche mashinani wakaazi wa Pwani hawafai kujitenga na mradi huo bali kushiriki kikamilifu
Seneta maalum Miraj Abdillahi amesema endapo wakaazi watajitenga na mchakato huo basi taifa hili litazidi kuathirika na makali ya ukame hali itakayoathiri zaidi maisha ya wananchi katika miaka ijayo.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Miraj amesema wananchi wanastahili kushiriki upanzi wa miti katika sehemu zao za makaazi na kisha baadaye kushirikiana na wadau wa kimazingira katika kuendeleza mradi huo katika maeneo mengine ya Ukanda wa Pwani.
Katika mradi huo uliyoanzishwa na Rais William Ruto wa upanzi wa miti bilioni 15 katika kipindi cha miaka 10 ijayo, Miraj ananuia kupanda miti milioni 2 katika ukanda wa Pwani.