Story by Gabriel Mwaganjoni-
Wakaazi wa ukanda wa Pwani wamehimizwa kuvuna maji katika sehemu zinazoshuhudia mvua ili wayatumie maji hayo katika shughuli ya uhifadhi wa mazingira.
Seneta mteule Miraj Abdilahi amesema hatua hiyo itasaidia pakubwa katika kupanda na kuikuza miti ambayo mwisho itadhibiti hali ya ukame katika ukanda huu na nchi nzima.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Miraj ameongeza kwamba harakati zake za upanzi wa miti milioni moja katika ukanda wa Pwani zimeshika kasi huku akisema kwamba mpango huo utawashirikisha vijana na akina mama vile vile.
Kiongozi huyo amehimiza ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kudhibiti makali ya ukame kwa kukumbatia upanzi wa miti mashinani.