Jumla ya shilingi milioni 36 fedha za hazina ya ustawi wa eneo bunge la Jomvu zimetumika kuwakimu wanafunzi wasiyobahatika katika kuwawezesha kuendelea na masomo.
Mbunge wa Jomvu Badi Tamesema jumla ya Wanafunzi 3,400 wa shule za upili na vyuo vikuu wamenufaika na mgao huo wa basari na wataendelea na masomo yao muhula wa tatu unapoanza.
Akizungumza katika eneo bunge lake la Jomvu, Badi amehoji kwamba jitihada hizo zitapelekea watoto waliyokuwa wamekata tamaa maishani kutokana na ukosefu wa karo kuendelea na masomo yao bila ya mahangaiko.
Badi hata hivyo amehoji kwamba kuna haja ya eneo bunge hilo kuwa na taasisi maalum ya kiufundi ili kuwawezesha Vijana kujikimu kwa ujuzi aina mbalimbali wa kujiajiri wenyewe.