Taarifa na Salim Mwakazi
Familia 43 katika eneo la Nguluku, Msambweni kaunti ya Kwale zinatarajiwa kuhamishwa ili kutoa nafasi kwa shughuli ya uchimbaji madini baada ya kupokea fidia ya ardhi zao kutoka kwa kampuni ya Base Titanium.
Afisa wa maswala ya kijamii katika kampuni hiyo, Pius Kassim amesema familia hizo ni miongoni mwa familia 52 zilizokubali kuhamishwa kutoka eneo hilo.
Pius aidha ameeleza kwamba kufikia sasa ni familia tatu pekee kutoka eneo hilo zilizowasilisha kesi mahakamani kupinga uhamisho huo.
Jumla ya shilingi milioni 270 zitatumika kuwafidia wakaazi watakaoathirika na shughuli hiyo ya uchimbaji madini katika eneo hilo la Nguluku.