Story by Janet Shume –
Baadhi ya mila na tamaduni za kiafrika ambazo zinaendelea kutekelezwa katika baadhi ya jamii zimetajwa kuwa chanzo cha ubaguzi wa Wanawake na uendelezaji wa dhulma za kijinsia.
Akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani yalioandawaliwa katika kaunti ya Kwale, Mratibu katika Tume ya kitaifa ya ardhi kaunti ya Kilifi Dkt Ummi Kugula amesema jamii inafaa kusitisha mila hizo zinazowakandamiza wanawake.
Dkt Ummi amesema wakati umefika sasa kwa wanawake kujitambua na kujitosa katika nyadhfa mbalimbali pasi na hofia lolote na kuifanya jamii kuamini juhudi zao.
Kwa upande wake Afisa wa Shirika lililoandaa hafla hiyo la NAYA, Dorcas Mwachi amewataka viongozi walio uongozini kaunti ya Kwale hususan Wanawake kupigania kupitishwa kwa mswada wa jinsia.