Picha kwa hisani –
Aliyekua gavana wa Nairobi mike Mbuvi sonko anatarajiwa kufika mbele ya maafisa wa idara ya DCI kuandikisha taarifa kuhusu madai aliyoyaibua dhidi ya katibu katika idara ya usalama Karanja Kibicho kwamba alihusika katika kupanga vurugu za baada ya uchaguzi wa mwaka 2017.
Idara ya DCI ilimtaka sonko kuandikisha taarifa baada ya Kibicho kulalamika kwamba mwanasiasa huyo ametuhumiwa kwa kupanga vurugu za baada ya uchaguzi wa mwaka 2017 ili kuchafulia jina chama pinzani cha ODM.
Hata hivyo aliyekua msaidizi wa Sonko, Ben Mulwa amedokeza kwamba sonko amehairisha kikao kati yake na maafisa wa DCI hadi siku ya jumatano juma hili.
Taarifa hio aidha imekinzana na ile ya maafisa wa DCI ambao wamesema mwanasiasa huyo atahojiwa hii leo kama ilivyopangwa.