Picha kwa hisani –
Mahakama ya Kiambu imeamuru aliyekua gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko azuiliwe kwa siku tano zaidi gerezani,kusubiri kikao cha mahakama cha siku ya jumanne juma lijalo kubaini iwapo ataachiliwa kwa dhamana.
Sonko ambae anakabiliwa na mashataka zaidi ya 12, alizuiliwa katika gereza la Kamiti usiku wa hapo jana,baada ya maafisa wa kitengo cha kupambana na ugaidi nchini ATPU, chini ya idara ya DCI kumfungulia mashtaka ya ugaidi.
Inspekta mkuu wa kitengo cha ATPU Newton Thimangu amesema wanataarifa zaidi za kijasusi zinazodhihirisha kwamba Sonko anafadhili makundi ya kigaidi ili kutatiza amani ya taifa hili,akitaka azuiliwe kwa siku 30 ili kukamilisha uchunguzi.
Kesi yake imeratibiwa kusikilizwa tena tarehe 9 mwezi huu wa februari ili kujua iwapo ataachiliwa kwa dhamana.