Picha kwa hisani –
Aliyekua gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko anazuiliwa katika gereza kuu la Kamiti kutoa nafasi kwa uchunguzi wa madai yanayomkabili ya kufadhili shughuli za ugaidi.
Hapo jana Sonko alihamishwa kutoka gereza la Gigiri hadi gereza hilo la Kamiti baada ya maafisa wa kitengo cha kupambana na ugaidi ATPU chini ya idara ya DCI kuwasilisha kesi ya ugaidi dhidi yake katika mahakama ya Kahawa magharibi.
Hii leo Sonko anatarajiwa kuwasilishwa mahakamani kujua hatima yake iwapo ataachiliwa kwa dhamana au ataendelea kuzuiliwa katika gereza hilo kwa siku thelathini kutoa nafasi ya uchunguzi kama walivyopendekeza maafisa wa DCI.
Siku ya Jumanne juma hili Sonko pia aliwasilishwa katika mahakama ya kiambu baada ya kuzuiliwa usiku mzima katika kituo cha polisi cha Muthaiga,akikabiliwa na mashataka 12 ikiwemo wizi wa mabavu na uharibifu wa mali madai ambayo aliyakana.