Story by Ali Chete-
Baraza la kitaifa linaloangazia maslahi ya watu wenye uwezo maalum likishirikiana naTume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC limeandaa mikakati ambayo itawezesha jamii hiyo kupiga kura kwa njia ya usalama.
Mratibu wa mipango wa baraza hilo katika kaunti ya Mombasa Juliet Ruwa amesema tayari baraza hilo limeweka mikakati ya kutosha ikiwemo vifaa vinavyotumiwa na jamii hiyo ili kuhakikisha watu wenye mahitaji maalum wanapiga kura bila ya kupata matatizo yoyote.
Juliet ameihimiza jamii hiyo sawa na wale wanaolenga kuwania nyadhifa mbalimbali za kisiasa kujitokeza na kujisajili kama wapiga kura katika afisi za IEBC.
Wakati uo huo amehimiza wakaazi wa kaunti ya Mombasa kuhakikisha wanazingatia swala la amani.