Story by Janet Shume –
Idara ya usalama eneo la Msambweni imethibitisha kupatikana kwa miili ya vijana wawili waliozama maji baharini katika eneo Gasi.
Afisa mkuu wa polisi eneo hilo Roy Nasio amesema kulingana na ripoti kamili vijana hao walikuwa watatu walipokwenda kuogelea baharini lakini wawili wakazama maji baada ya kushindwa mawimbi makali ya bahari huku mmoja akinusurika kifo.
Nasio amewahimiza wakaazi kuchukua tahadhari nyakati zote wanapoelekea baharini kuogelea ili kudhibiti.
Miili ya vijana hao inahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Kwale