Mkufunzi wa timu ya taifa ya soka Harambee Stars Sebastien Migne amefanya mzoezi ya kwanza na kikosi cha wachezaji 21 katika maandalizi ya mechi dhidi ya Ghana iliyoratibiwa kuchezwa Jumamosi hii.
Harambee Stars inakutana na Ghana katika mechi ya kufuzu kwa mchuano wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Kulingana na Migne ni kuwa wachezaji wapo katika kiwango kizuri.
Kenya imepangwa katika kundi F pamoja na Sierre Leone, Ethiopia na Ghana.
Mchuano wa AFCON mwaka 2019 utafanyika mwezi June nchini Cameroon.